Jua Haki ZakoAuthor: RFI Kiswahili
Jua Haki Zako ni makala yanayokuelimisha juu ya umuhimu wa kufahamu haki zako na sheria halali zilizomo kwenye jamii, mataifa na dunia kwa ujumla. Jua Haki Zako itakuelimisha juu ya masuala mbalimbali ya kisheria ndani ya Afrika Mashariki, Afrika na Duniani kwa ujumla. Language: sw Genres: Government Contact email: Get it Feed URL: Get it iTunes ID: Get it |
Listen Now...
Kenya: Uhuru wa kutumia mitandao ya kijamii na mipaka yake
Thursday, 9 January, 2025
Siku ya Jumatatu asubuhi Vijana wanne kati ya 6 waliotekwa nyara katika wiki za hivi majuzi waliachiliwa huru, saa chache kabla ya maandamano yaliyopangwa kufanyika kupinga kutoweka kwao. Billy Munyiri Mwangi na Peter Muteti waliungana na familia zao huko Embu na Nairobi, mtawalia, baada ya kuzuiliwa kwa zaidi ya wiki mbili ilhali Rony Kiplangat alipatikana katika kaunti ya Machakos naye Benard Kavuli akapatikana katika maeneo ya Kitale magaribi mwa nchi. Katika makala Jua haki zako, tunaangazia huru wa kutumia mitandao ya kijamii na katika kutumia mitaoa hiyo kuna mipaka yake. Je nchini Kenya hatua zipi zinafaa kuchukuliwa ikiwa mshukiwa atapatikana na hatia ya kukiuka huru ywa mitandao ya kijamii.